Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA – Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Qur’an Tukufu: فَإِنَّ حِزْبَ اللَّهِ هُمُ الْغَالِبُونَ / (سورة المائدة، آیة ۵۶) / Hakika kundi la Mwenyezi Mungu – hao ndio washindi (Surat Al-Maidah: Aya ya 56).
Aya hii tukufu inaashiria kwamba wale wanaoshikamana na njia ya haki, chini ya uongozi wa Mwenyezi Mungu na waliowekwa na Yeye (swt), wakifuata misingi na maelekezo safi ya Kidini, watashinda daima, hata kama kidhahiri watakabiliwa na dhulma, mateso au mashinikizo ya kimataifa.
Katika muktadha wa kisasa, mashujaa wa Muqawama kama vile Hezbollah, Ansarullah, Hamas, na vikundi vingine vya upinzani wa Kiislamu, huonekana kuwa ni mionekano hai ya maana ya "حزب الله" – wanaoongoza mapambano dhidi ya dhulma na utawala dhalimu.
Ufafanuzi zaidi: Katika Aya hii, Mwenyezi Mungu (swt) anatujulisha kuwa wale waliomo katika "Hezbollah" — yaani kundi linalomtii Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na waliokuwa waumini wa kweli — ndio washindi wa kweli, si kwa nguvu za kijeshi tu, bali kwa ushindi wa haki juu ya batili, na ushindi wa uadilifu juu ya dhulma.
Maelezo Mafupi ya Tafsiri ya Aya Hii Tukufu:
- "Hezbollah" humaanisha: Kundi lililojifunga na miongozo ya Mwenyezi Mungu, linalosimama na kutetea haki, hata likiwa ni dogo au linakabiliwa na maadui wakubwa.
- Aya hii imekuwa nembo ya Harakati za Muqawama (Upinzani wa Kiislamu) kama vile Hezbollah ya Lebanon, Ansarullah ya Yemen, na wengineo wanaopambana dhidi ya dhulma ya mabeberu ya Kimataifa.
- Ushindi unaozungumziwa hapa si lazima uwe wa papo kwa papo au wa kijeshi tu, bali pia unaweza kuwa ni ushindi wa Ujumbe wa Haki, uimara wa msimamo, na hatimaye ushindi wa kiroho na wa kihistoria. Na hiki ndio kinachotokea leo hii nchini Yemen baada ya Mabeberu Marekani na washirika wake kushindwa vibaya mbele ya wapambanaji na watetezi wa Palestina, Ansarullah wa Yemen.
Your Comment